Jumatano 6 Mei 2026 - 22:40
Umoja wa Kiislamu, muqawama na diplomasia ya nishati ni nguzo tatu za kubadilisha mizani ya dunia

Hawza/ Sheikh Ismail Bazdar, khatibu wa Ijumaa wa Ahlus-Sunnah wa Bushehr Iran, katika kipindi cha “Upeo wa Ushindi” cha Majma’ ya Kimataifa ya Qadimun alisisitiza kwamba; umoja wa Kiislamu, muqawama na diplomasia ya nishati ni nguzo kuu tatu za kubadilisha mizani ya dunia.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, kipindi cha televisheni “Upeo wa Ushindi; Mwisho wa tawala ya Marekani na Kuibuka kwa Mpangilio Mpya wa Dunia” kilifanyika siku ya Jumatatu tarehe 4 May kwa juhudi za Majma’ ya Kimataifa ya Qadimun, kwa ushiriki wa kundi la shakhsia za kidini na kisiasa kutoka nchi mbalimbali, na kilirushwa kupitia vituo vya televisheni ya Al-Kawthar na Safir.

Sheikh Ismail Bazdar, khatibu wa Ijumaa wa Ahlus-Sunnah wa mji wa Bushehr, mwanzoni mwa hotuba yake huku akirejelea mabadiliko makubwa katika mfumo wa dunia alisema: Dunia ya leo iko katika hatua ya kuvuka kipindi ambacho kinaweza kupelekea mwisho wa zama fulani za mifumo ya awali ya nguvu na kuibuka kwa mizani mpya, na katika hali hii, Ummah wa Kiislamu unaweza kuwa na nafasi yenye athari kubwa.

Akaeleza kwamba; dhana ya “kushindwa” katika muktadha huu haijafungamana tu na upande wa kijeshi, na akaongeza: Suala hili linajumuisha vipengele mbalimbali vikiwemo nyanja za kiuchumi, kisiasa na kitamaduni, na kulichambua kunahitaji mtazamo mpana na wa pande nyingi.

Khatibu wa Ijumaa wa Bushehr aliendelea kubainisha kwamba; “Umoja wa Kiislamu” ni moja ya nguzo kuu katika njia hii, na akasisitiza: Muafaka wa kiuchumi kupitia kuendeleza ushirikiano wa kibiashara, kuanzisha mifumo ya kifedha ya pamoja na kupanua mwingiliano wa pande nyingi kunaweza kusaidia kuimarisha nafasi ya nchi za Kiislamu katika uwanja wa kimataifa.

Bazdar pia alisisitiza umuhimu wa uratibu wa kisiasa kati ya nchi za Kiislamu na akasema: Kuundwa kwa misimamo ya pamoja katika nyanja za kimataifa kunaweza kuwa na nafasi katika kuongeza uwezo wa majadiliano na ushawishi wa ulimwengu wa Kiislamu.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, alirejelea nafasi ya “mhimili wa muqawama” na kuuchukulia kuwa ni sababu yenye athari katika kubadilisha baadhi ya mizani ya uwanjani, na akaongeza: Mabadiliko ya miaka ya hivi karibuni yameonesha kwamba; wahusika wa kikanda wanaweza katika hali fulani kuathiri mwenendo uliopo.

Khatibu huyu wa Ijumaa wa Bushehr aliendelea kwa kurejelea “diplomasia ya nishati” kama mojawapo ya nyenzo muhimu za nguvu na akasema: Rasilimali za nishati na njia za usafirishaji wake ni miongoni mwa uwezo muhimu ambao, endapo utasimamiwa kwa usahihi, unaweza kuwa na athari katika kuimarisha uhuru wa kiuchumi na kisiasa wa nchi.

Mwishoni, akisisitiza juu ya umuhimu wa kuwa macho mbele ya changamoto na kutumia vyema fursa zilizopo, alielezea matumaini yake kwamba; ulimwengu wa Kiislamu utaweza kwa kutegemea uwezo wake, kuchukua nafasi iliyo hai zaidi katika kuunda mustakabali wa mfumo wa kimataifa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha